
Tatizo la kukosa hamu ya kufanya mapenzi au kukosa nyege kwa lugha ya
mitaani huwatokea zaidi wanawake kuliko wanaume lakini ni wanaume
wanaokerwa zaidi na tatizo hili kulio wanawake. Wakati ambapo ni
asilimia 15 hadi 16 ya wanaume wenye tatizo hili, idadi ya wanawake ni
mara mbili ya hii ya wanaume. Lakini wakati ni asilimia 23 ya wanaume
wanaonyesha kuridhika kuishi na tatizo hili, asilimia 46 ya wanawake
wapo radhi kabisa kuendelea kuishi na tatizo hili.
Si lazima kuendelea kuishi na tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo
la ndoa kwa sababu kuna mambo mengi unayoweza kuyafanya ili kuondokana
na hili tatizo.
Hali ya kupenda kufanya mapenzi au tendo la ndoa kwa mwanamke
inabadilikabadilika sana ikipanda na kushuka kulingana na matukio
mbalibali yanayomtokea katika maisha yake. Baadhi ya matukio
yanayoathiri hamu ya mwanamke kufanya mapenzi ni pamoja na kuanza na
kwisha kwa mahusiano ya kimapenzi na mwanamme, kupata ujauzito, na
magonjwa. Kama wewe mwanamke umepatwa na ha hii unaweza kukabiliana nayo
kwa kubalisha jinsi unavyoishi, kufanya mambo kadhaa yatakayo badilisha
hali hii au kutumia baadhi ya dawa zinazosaidia kuondoa tatizo hili.
Jee, Utajuaje kama Una Tatizo?
Kuna vitu vingi ukiviona vinakutokea, ujue una tatizo hili la kukosa
hamu ya kufanya mapenzi.Tulivijadili viashiria hivi kwa kina
tulipozungumzia tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa
wanaume. Unaweza kusoma tulivyojadili kwa kusoma ukurasa huu “Mwanamme Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa.”

Sababu Za Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa
Sababu zinazoweza kupelekea mwanamke kukosa hamu ya kufanya tendo la
ndoa ni nyingi lakini kwa ujumla karibu zote tunaweza kuzigawanya katika
makundi manne:
1. Mahusiano Baina Ya Mwanamke Na Mwanamme
Kwa wanawake walio wengi ukaribu wa kihisia
ndicho kitu cha kwanza katika kujenga mapenzi kati yake na mwanamme.
Hivyo, mahusiano mabovu yaweza kuwa ndicho chanzo cha kukosa hamu ya
kufanya tendo la ndoa kwa mwanamke. Mwanamke atakosa hamu ya kufanya
mapenzi endapo hakutokuwa na mawasiliano baina yake na mumewe, kutakuwa
na migogoro kati yake na mumewe isiyokwisha, kutakuwa na ukosefu wa
mawasiliano kuhusu mahitaji yake ya kufanya mapenzi na jinsi ambavyo
yeye angependa kufanyiwa kimapenzi na kama atahisi kuna ukosefu
wa uaminifu katika ndoa au mahusiano yao.
2. Matatizo Katika Maisha Yako
Matatizo
mbalimbali katika maisha ya mwanamke humsababishia kukosa hamu ya
kufanya mapenzi. Baadhi ya matatizo ambayo huweza kusababisha mwanamke
kukosa hamu ya kufanya mapenzi ni pamoja na magonjwa, mabadiliko katika
mwili wake na hata matumizi ya baadhi ya madawa:
Matatizo Katika Kufanya Tendo La ndoa. Kama
mwanamke anapata maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa au kama
mwanamke anakosa kufika kileleni, hali hii inaweza kusababisha akakosa
kabisa hamu ya kufanya mapenzi.
Matatizo ya afya. Magonjwa mengi husababisha
mwanamke akose hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baadhi ya magonjwa ni
maumivu ya viungo vya mifupa (arthritis), kansa, ugonjwa wa kisukari,
high blood pressure, matatizo katika mishipa ya damu ya arteri na
matatizo ya akili.
Matumizi ya madawa. Baadhi ya madawa
yakitumiwa, huondoa kabisa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke. Mfano
wa dawa hizo ni madawa ya kukabiliana na msongo wa mawazo.
Mtindo wa maisha. Matumizi ya pombe kuzidi kiwango, uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya huathiri hamu ya kufanya mapenzi.
Upasuaji. Upasuaji uliofanyika katika
maeneo ya maziwa au katika maeneno ya viungo vya uzazi humbadilishia
mwanamke mwonekano wake, huathiri ufanyaji kazi wa viungo hivyo na
mwisho kuathiri hamu yake ya kufanya mapenzi.
Uchovu. Uchovu unaotokana na kulea watoto wadogo au vikongwe huweza kuathiri hamu ya mwanamke ya kufanya mapenzi.
3. Mabadiliko Katika Mfumo Wa HomoniKukoma Hedhi.Mabadilko
ya viwango vya homoni katika mwili wa mwanamke yanaweza kusababisha
kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke. Kupungua kwa Estrogen
katika mwili wa mwanamke katika kipindi cha kuelekea kukoma hedhi
kunaweza kusababisha ukosefu wa hamu ya kufanya mapenzi. Upungufu wa
homoni hiyo husababisha uyabisi wa wa viungo vya sehemu nyeti na
kusababisha maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Mwanamke pia huweza kuwa na upungufu wa homoni ya testosterone,
homoni ambayo husaidia kuongeza hamu ya kufanya mapenzi kwa wanaume na
wanawake, hivyo mwanamke huyo akapungukiwa na hamu ya kufanya mapenzi.
Pamoja na kuwa wanawake wengi huendelea kupata hamu ya kufanya
mapenzi baada ya kukoma hedhi, baadhi kupungukiwa na hamu hiyo baada ya
mabadiliko haya ya viwango vya homoni katika miili yao.
Ujauzito na kunyonyesha. Mabadiliko katika mfumo wa
homoni wakati wa ujauzito, baada ya kujifungua na wakati wa kunyonyesha
huweza kusababisha mwanamke kukos hamu ya kufanya tendo la ndoa.
4. Matatizo Ya Kisaikolojia
Matatizo ya kisaikolojia yana mchango katika kumfanya mwanamke akose
hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baadhi ya mtatatizo hayo ni:
- Waswasi na kuwa na msongo wa mawazo
- Kuwa na mawazo mengi kuhusu matatizo ya kifedha au kikazi
- Kuhisi kutothaminiwa katika jamii
- Kuwa na historia ya kunyanyaswa kimwili au kijinsia kama kupigwa au kubakwa
- Kuwa na historia mbaya ya kimapenzi
-
Njia Za Kuondoa Tatizo La Kukosa Hamu Ya kufanya Tendo La Ndoa
Hakuna dawa ya moja kwa moja toka hospitalini kwa sasa hivi kwa ajili ya kuondoa tatizo hili, hata hivyo wanawake wengi wanaweza kurudi kwenye hali zao za kawaida kwa kushirikiana na waume zao waelewa. Jaribu kufanya mambo tuliyoyadokeza katika mada yetu ya “Mwanamme Kukosa hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa” ukisaidiana na mumeo. Unahitaji kuchunguza taratibu na kwa kina chanzo cha tatizo lako, na taratibu lifanyie kazi kwa msaada wa mume wako.Katika nchi zilizoendelea, kila siku wamekuwa wakija na dawa na vifaa vipya vya kuondoa tatizo hili na vingi bado ni vya bei kubwa na/au vinapatikana kwa shida. Vipo ambavyo vimeonyesha mafanikio makubwa, mifano ya vitu hivyo ni Suction Vibrators, Desire Creams na Erection Drugs.Unaweza kupata mafanikio makubwa (wasomaji wangu wengi wamefanikiwa na kunishukuru) kwa kutumia chakula kinachosaidia kuongeza hamu au kwa kutengeneza na kutumia viagra asilia. Hivi nimevielezea hapa chini. Kama hivi bado havijakusaidia, nashauri utumie virutubisho vya mwili ambavyo husamabazwa na makampuni mbalimbali. Vipo vinavyofanya kazi kwa haraka na kutibu kabisa tatizo hili. Endapo umepata tatizo kutambua virutubisho vizuri vya kutumia, wasiliana nasi kwa kutumia njia yo yote iliyo rahisi kwako kati ya hizi nilizoziorodhesha chini ya ukurasa huu.Chakula Cha Kuongeza Hamu Ya Mapenzi
Utafiti umeonyesha pasi shaka kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya chakula tunachokula na afya ya viungo vya uzazi. Baadhi ya chakula na virutubisho vimehusishwa na hamu ya kufanya mapenzi (nyege). Vitubisho ndani ya chakula ambavyo vinasaidia hali hiyo ni antioxidants, vitamin C, vitamin E, potassium na zinc. Kirutubisho cha zinc kinaongeza mbegu kwa mwanamme (sperm count) hivyo humsaidia kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa. Chakula cho chote chenye virutubisho hivi vikiliwa humfanya mlaji asikie hamu ya kufanya mapenzi au kwa maneno ya mtaani, chakula hiki kinasaidia kuongeza nyege. Baadhi ya chakula cha kuongeza nyege ni:Tikitimaji-Hili linachukuliwa kuwa ndilo tunda bora katika kuboresha afya ya mapenzi. Tunda hili lina asilimia 92 ya maji na asilimia 8 zinazobakia zina phytonutrient citrulline ambayo hugeuzwa kuwa arginine. Arginine ni amino acid ambayo hufanya mishipa ya damu kuwa kwenye hali ya ubora wake na kusadia damu kupita vizuri zaidi. Tikitimaji kwa hiyo husaidia damu ifike kwa kiwango kizuri zaidi kwenye sehemu ambazo hutakiwa kutanuka wakati mtu akipata hisia za kufanya tendo la ndoa ambazo ni viungo vya ndani ya kisimi cha mwanamke na ndani ya uume wa mwanamme.Strawberries– matunda haya yana antioxidants kwa kusaidia afya ya moyo na mishipa ya damu (arteri) na vitamin C ambayo huongeza kiwango cha mbegu kwa mwanamme.Pombe-glasi moja ya mvinyo hukufanya uwe na akili tulivu. Pombe kwa kiwango kikubwa huleta kinyume cha matarajio na kuondoa kabisa hamu ya mapenzi.Avocadro-tunda hili lina vitamini E ambayo ni antioxidant. Ndani ya tunda hili kuna potassium na vitamini B6 ambavyo huboresha afya ya moyo na kusaidia mzunguko wa damu.Viazi vitamu-hivi vina potassium ambayo husaidia kuondoa tatizo la high-blood pressure.Chakula kingine katika kundi hili ni broccoli (picha hapa chini), karafuu, mayai na tangawizi.Kuna mchanganyiko wa matunda ukisagwa pamoja na kunywewa umeonyesha kuongeza hamu ya kufanya mapenzi au kuongeza nyege. Nilionyesha namna mbili za kutengeneneza mchanganyiko huo na nikauita “Viagra asilia.” Nitaongeza mchanganyiko wa tatu wenye matunda mengi zaidi ili uweze kuchagua ule utakaoona ni rahisi zaidi kuutengeneza.Jinsi Ya Kutengeneza Viagra Ya Asili
Kusanya matunda kama yanavyoonyeshwa kwenye video hii hapa chini, saga kwa pamoja katika blender na kisha kunywa glasi moja ya mchanganyiko huo. Hakuna kipimo kamili cha kutumia, lakini ukipata glasi tatu kwa siku utapata mabadiliko ya kutosha kabisa. Wapo watu wengi waliofuata ushauri huu, wakanipigia simu kuwa hali zao zimekuwa nzuri sana baada ya kutumia kinywaji hiki. Jaribu kisha nipe matokeo.Kama umeshindwa kupata matunda yote kwa kutengeneza viagra hii asilia, nenda ukurasa wa “Mwanamme Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa” ambamo nimeelezea viagra asilia ya matunda mawili tu, tikiti maji na limau.Kama una swali lolote au maoni yako kuhusiana na mada hiyo hapo juu, usisite kutuandikia. Pia usisite kuomba ushauri zaidi pale ulipojaribu njia hizi ukakwama mahali.